Matthew 20:25-28

25Lakini Isa akawaita wote pamoja na kuwaambia, “Mnafahamu kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, nao wenye vyeo huonyesha mamlaka yao. 26 aIsiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote anayetaka kuwa mkuu miongoni mwenu hana budi kuwa mtumishi wenu, 27 bnaye anayetaka kuwa wa kwanza miongoni mwenu hana budi kuwa mtumwa wenu: 28 ckama vile ambavyo Mwana wa Adamu hakuja ili kutumikiwa, bali kutumika na kuutoa uhai wake uwe fidia kwa ajili ya wengi.”

Isa Awaponya Vipofu Wawili

(Marko 10:46-52; Luka 18:35-43)

Copyright information for SwhKC